Wagogo) ni
kabila la
Tanzania ya kati, wenyeji wa mikoa ya
Dodoma na
Singida.
Lugha yao ni
Cigogo (kwa
Kiswahili hutamkika
Kigogo).
Dini ya wengi wao ni
Ukristo, hasa wa
madhehebu ya
Anglikana, halafu wa
Kanisa Katoliki.
Historia ya Wagogo inaweza kuelezeka kwa kuangalia yafuatayo:
Utawala wa
jadi,
nyumba za asili,
chakula kikuu na
lafudhi ya lugha.
Utawala wa Jadi
Wagogo walikuwa wakiongozwa na mtu mmoja aliyeitwa
Mtemi. Watemi kadhaa waliongoza kabila hilo kabla ya mfumo wa uongozi kuvurugwa na
ukoloni. Mtemi wa mwisho aliitwa
Mazengo ambaye alitokea katika
kijiji cha
Mvumi,
wilaya ya Dodoma vijijini.
Nyumba za asili
Wagogo wamekuwa wakijenga nyumba ambazo huitwa "
tembe". Tangu zamani kuta za tembe zilijengwa kwa fito (sito kwa lugha yao) zilizosukwa kwa kupisha kuzuia mwanga na maji. Vipande vya kuta vilivyosukwa kwa sito vinaitwa "izizi". Tembe huezekwa kwa udongo ambao hushikiliwa na miti midogomidogo (walo). Walo huwa unashikiliwa na miti mikubwa kidogo (mahapa) na mahapa hushikiliwa na miti mikubwa (Michichi). Michichi ambayo ndiyo hubeba uzito wote hushikiliwa na nguzo kubwa za miti imara na migumu. Nguzo hizo hutiwa masumbiri. Kwa miaka ya karibuni na hata sasa kuta za tembe hujengwa na matofali yanayotengenezwa kwa udongo.
Chakula kikuu
Wagogo hula
ugali wa
uwele kama chakula kikuu na huchukulia ugali wa
mahindi kama mwepesi. Miaka ya zamani mlo wa kawaida wa Mgogo mwenye uwezo (yaani mwenye
ng'ombe) ulihusisha ugali,
maziwa,
mafuta ya ng'ombe, na
mboga kama
mlenda,
safwe,cidungulilo,nyakifwega, mhilile,sanghala,mnzimwe,cipali,ihaji,sagulasagula,ikuwi (hasa wakati masika inapoanza) n.k. Kwa miaka ya sasa Wagogo wamekuwa wakila chakula cha kawaida kama makabila mengine nchini Tanzania.
Lugha
kabila la Wagogo lina makabila mengine madogomadogo ndani yake. Wao hutofautiana kwa jinsi ambavyo hutamka maneno au huongeza na kupunguza baadhi ya matamshi kwenye neno. Moja ya makundi yanayoonekana wazi kwenye kabila hili ni kama Wanyambwa ambao huongea lafudhi ya Kinyambwa. Wanyambwa hutokea vijiji vya magharibi mwa
mji wa
Dodoma. Wengine ni Wanyaugogo ambayo huongea lafudhi iitwayo Chinyaugogo. Wanyaugogo ambao ndio wanaowakiLisha kundi kubwa sana hutokea vijiji vya mashariki na kusini mwa mji wa Dodoma na pia
Mpwapwa.
Majina ya ukoo ya Kigogo
majina hayo ni kama Mazengo, Kidosa, Cilongani, Malecela, Mwaluko, Mavunde, Ndejembi, Manyesela, Mbogambi, Mdachi, Kapaya,Matonya, Mtunya, Kusila, Nhonya,Mhalanyuka, Mbenaa, Chibile, Mdoli, Lusinde,Njamasi,Majenda,Chiwamba,Mazoya,Ufinyu,Chilyawanhu,Magaya, Ngoli,Chiwanga,Lubeleje,Makupila,Fukunyi (endeleza
No comments:
Post a Comment